MADIWANI DAR, WATAKIWA KUWATUMIKIA WANANCHI
Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za mitaa TAMISEMI Mhe Profesa Riziki Shemdoe amewataka madiwani wa Halmashauri za Mkoa wa Dar es salaam kutambua kuwa wao wapo kwa ajili ya wananchi na wamechaguliwa na wananchi hivyo wanapaswa kuwatumikia wananchi kwa kuwaletea maendeleo na kuwaimarishia huduma muhimu za kijamii
Akizungumza jijini Dar es Salaam katika ufunguzi wa mafunzo ya madiwani wa Mkoa wa Dar es salaam yaliyoandaliwa na ofisi ya CAG kuhusu uendelezaji na usimamizi wa rasirimali za Halmashauri, mafunzo ambayo yamefanyika kwenye ukumbi wa APC Hotel Mbweni, Waziri wa Nchi ofisi ya waziri mkuu tawala za mikoa na Serikali za mitaa TAMISEMI Profesa Ziziki Shemdoe amesema madiwani wa halmashauri zote za mkoa huo wanapaswa kutambua kuwa wao wapo kwa ajili ya wananchi, wamechaguliwa na wananchi na hivyo wanapaswa kuwatumikia wananchi
Profesa Shemdoe amesema Halmashauri za Mkoa wa Dar es Salaam ndio zenye kiwango kikubwa cha ukusanyaji wa mapato ukilinganisha na Halmashauri zingine hivyo ni muhimu kuwa na matumizi bora ya rasilimali fedha zimazokusanywa ili kuwawezesha wamanchi kupata huduma bora za kijamii ikiwemo afya ambapo pia amewataka kuweka mipango ya kujitegemea kifedha badala ya kutegemea fedha kutoka serikali kuu huku pia akizungumzia fursa ya Halmashauri hizo kukopa kwenye benki ili kuboresha huduma za kijamii
Aidha muandaaji wa mafunzo hayo ambaye ni Mdhibiti na Mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali CAG, CPA Charles Kichere amesema mafunzo hayo ni muhimu katika kuwawezesha madiwani kutekeleza wajibu wao kwa ufanisi kwa kuzingatia thamani ya fedha
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila amesema ipo changamoto kwa Halmashauri kupata hati chafu kutokana na uelewa mdogo kwenye masiala ya fedha hivyo mafunzo hayo yatawaimarisha katika nidhami ya matumizi ya fedha za Halmashauri
Baadhi ya madiwani walioshiriki mafunzo hayo wameeleza namna ambavyo mafumzo hayo yatawaimarisha kwenye nidhamu ya fedha huku wakizungumzia fursa iliyotolewa na waziri wa TAMISEMI kwa halmashauri zenye mapato makubwa kuweza kupata mikopo kwenye mabenki kuboresha huduma za jamii



Comments
Post a Comment