MKURUGENZI WA LATRA AFURAHISHWA NA NJIA ZA USAMBAZAJI TAARIFA ZA HALI YA HEWA.



Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini LATRA, Habibu Suluo, amepongeza ubunifu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) katika kusambaza taarifa za hali ya hewa kwa wananchi kupitia njia mbalimbali za mawasiliano, hususan mitandao ya kijamii ikiwemo WhatsApp Channel, na kujiunga na jukwaa hilo alipofika katika banda la TMA kwenye Maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayoendelea katika Viwanja vya Chinangali Park jijini Dodoma.

Akizungumza baada ya kupata maelezo kuhusu huduma zinazotolewa na TMA, Suluo alisema matumizi ya majukwaa ya kidijitali yameongeza upatikanaji wa taarifa za hali ya hewa kwa wakati na kuwafikia wananchi wengi zaidi kwa urahisi.

TMA inawakaribisha wananchi kutembelea banda lake kesho wakati wa kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa
Umma 2026 ili kupata elimu zaidi kuhusu huduma na bidhaa mbalimbali za hali ya hewa pamoja na namna ya kufikia taarifa hizo kupitia mifumo ya kidijitali inayotolewa na mamlaka hiyo.


Comments

Popular posts from this blog

RC CHALAMILA AWATAKA WENYEVITI NA WATENDAJI KATA NA MITAA DAR KUSIMAMIA ULINZI NA USALAMA.

MAHAFALI YA NANE SHULE YA AWALI NA MSINGI SAI YAFANA, WAZAZI WATAKIWA KULEA WATOTO KATIKA MISINGI YA MAADILI MEMA.