TMA YAENDELEA KUJENGA UELEWA WA MASUALA YA HALI YA HEWA KATIKA WIKI YA UTUMISHI WA UMMA 2026


Dodoma, 

 Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imeendelea kuwajengea wananchi uelewa kuhusu masuala mbalimbali ya hali ya hewa kupitia ushiriki wake katika Maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayoendelea kufanyika katika viwanja vya Chinangali Park jijini Dodoma.

Maonesho hayo yanayofanyika kuanzia Juni 16 hadi 23, 2026, yanalenga kutoa elimu na kuhamasisha wananchi kuhusu huduma zinazotolewa na taasisi mbalimbali za umma. Ufunguzi rasmi wa maadhimisho hayo ulifanywa Juni 17, 2026 na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Ridhiwani Kikwete.

Kupitia banda lake, TMA imekuwa ikitoa elimu kwa wananchi kuhusu namna ya kusoma na kutafsiri taarifa za hali ya hewa pamoja na matumizi yake katika sekta mbalimbali muhimu za uchumi na maendeleo.

Wananchi wanaotembelea banda hilo wanapata fursa ya kujifunza jinsi taarifa za hali ya hewa zinavyoweza kusaidia katika kupanga na kuboresha shughuli za kilimo, usafiri, uvuvi na sekta nyingine zinazotegemea hali ya mazingira kwa kiasi kikubwa.

TMA imeeleza kuwa matumizi sahihi ya taarifa za hali ya hewa yana mchango mkubwa katika kupunguza athari zitokanazo na mabadiliko ya tabianchi na kuongeza ufanisi wa shughuli za kijamii na kiuchumi.

Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma mwaka huu yanaongozwa na kaulimbiu isemayo “Kuchochea Uwajibikaji Jumuishi kwa Huduma Endelevu,” ikisisitiza umuhimu wa taasisi za umma kutoa huduma bora, zinazowajibika na zinazokidhi mahitaji ya wananchi.




Comments

Popular posts from this blog

RC CHALAMILA AWATAKA WENYEVITI NA WATENDAJI KATA NA MITAA DAR KUSIMAMIA ULINZI NA USALAMA.

MAHAFALI YA NANE SHULE YA AWALI NA MSINGI SAI YAFANA, WAZAZI WATAKIWA KULEA WATOTO KATIKA MISINGI YA MAADILI MEMA.