TMA YATOA ANGALIZO LA HALI MBAYA YA HEWA NA UPEPO MKALI UKANDA WA PWANI.

 





Mamlaka ya hali ya hewa Tanzania (TMA)imetoa angalizo la hali mbaya ya hewa hasa upepo mkali katika ukanda wa pwani ya Bahari ya Hindi, likiwatahadharisha wananchi kuhusu uwezekano wa mabadiliko ya hali ya hewa yenye athari katika siku zijazo.


Kwa mujibu wa taarifa hiyo, baadhi ya maeneo yanayotarajiwa kuathirika ni maeneo ya ukanda wa pwani ya kaskazini mwa bahari ya Hindi (mikoa ya Tanga, Dar es Salaam na Pwani (ikijumuisha visiwa vya Mafia)) pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba.


Mamlaka hiyo imeeleza kuwa hali hiyo inaweza kuambatana na upepo mkali unaoweza kufikia takribani kilomita 40 kwa saa, mawimbi makubwa ya bahari na hali ya kutokuwa tulivu kwa shughuli za baharini.


Wananchi, hususan wavuvi na wasafiri wa baharini, wameshauriwa kuchukua tahadhari na kuepuka shughuli za baharini zisizo za lazima ili kujikinga na hatari zinazoweza kujitokeza.


Hata hivyo wananchi wamehimizwa kufuatilia taarifa rasmi za hali ya hewa kutoka katika mamlaka hiyo kwa ajili ya maelekezo na tahadhari zaidi.

Comments

Popular posts from this blog

RC CHALAMILA AWATAKA WENYEVITI NA WATENDAJI KATA NA MITAA DAR KUSIMAMIA ULINZI NA USALAMA.

MAHAFALI YA NANE SHULE YA AWALI NA MSINGI SAI YAFANA, WAZAZI WATAKIWA KULEA WATOTO KATIKA MISINGI YA MAADILI MEMA.