WATANZANIA WAHIMIZWA KUCHANGIA DAMU KWA HIARI KUELEKEA SIKU YA MCHANGIA DAMU DUNIANI JUNI 14.
Meneja wa Program wa Mpango wa Taifa wa Damu Salama, Dkt. Lelo Baliyima, amewahimiza Watanzania kujitokeza kwa wingi kuchangia damu kwa hiari ili kusaidia kuokoa maisha ya wagonjwa wanaohitaji huduma hiyo hospitalini.
Amesema Tanzania imefanikiwa kukusanya asilimia 71 ya lengo la damu kwa mwaka wa fedha 2024/2025, huku asilimia 60 ya wachangiaji wakiwa ni watu wanaochangia baada ya ndugu au jamaa zao kuhitaji damu.
Dkt. Baliyima amesisitiza umuhimu wa kujenga utamaduni wa uchangiaji wa damu wa mara kwa mara kuelekea Maadhimisho ya Siku ya Mchangia Damu Duniani yanayofanyika Juni 14 kila mwaka.

Comments
Post a Comment